AFRICHINA AND RUMAFRICA DESTINATION INVESTMENT LIMITED

BRIEF INTRODUCTION.

BRIEF INTRODUCTION.

Africhina Destination Investment Limited was conceived since 2005 in Guangzhou (People Republic of China). It is a privately owned company with its scope in, design and printing, procurement agency, general supply and logistics.

The company was officially registered in Tanzania as a Limited Liability Company and incorporated under the Company Act 2002 with Incorporation Certificate No. 63114. The company is registered with Tanzania Revenue Authority (TRA) and issued with Certificates; Tax Identification Number (TIN) 106-300-275, VAT Registration Number (VRN) 40-001202-C, also hold valid business license B No.01129901, 01129695 and 01095203 for Procurement Agency, Printing and Textile products respectively.

 

Professional expertise, experience in both local, international market and sources gave us unique competitive edge in terms of price, quality and delivery time. Working together with our customer as one team/partner instead of working for them also has added greet satisfaction to all our esteemed customer, especially when it come to the need to design particular product to meet special requirement.

Wednesday, June 13, 2012

MPIGIE KURA CHRISTINA SHUSHO, IPIGIE KURA TANZANIA, IINUE AFRICA
VIVA SHUSHO....VIVA TANZANIA
Christina Shusho,akihojiana na mablogaz wa Kitanzania katika hotel ya The Atriums iliyoko Sinza Africa sana
Siku ya jana jioni mablogaz wanaomiliki blogu za Kikristo Tanzania, Rulea Sanga, Uncle Jimmy, Sam Sasali, K-Junior, Martin Macele walikuwa na mahojiano na Christina Shusho katika hotel ya The Atriums Sinza Africasana kuhusiana na shindano kubwa lililoko machochoni pa mtumishi wa Mungu Christina Shusho.

Christina Shusho alimshukuru Mungu kwa kuweza kumtumia kama chombo kufikisha ujumbe kwa jamii kwa njia ya uimbaji na pia kuweza kushiriki katika Gospel Music Awards Africa. Pia aliwashukuru mablogaz kwa kazi yao nzito wanayofanya kumtangaza katika blogs zao na kupoteza muda wao kwaajili ya kumuinua Kristo.
Aliwaomba Watanzania na Africa nzima kumchangua Christina Shusho ili kuliwakilisha Bara la Africa,Tanzania na kumuweka Kristo juu ya vyote.
Christina Shusho ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na amekuwa chachu kwa waimbaji wenzake na kwa watanzania kwa uimbaji wake na ujumbe naoutoa ambao umekuwa na mguso katika kukarabati imani za watu.
Christina Shusho anategemea ku-perform DAR LIVE siku ya jumapili, kwahiyo amewaomba Watanzania wote kufika mahali pale na kuweza kumpigia kura, kutakuwepo na mablogaz na kompyuta zao ambapo utakutana nao na watakuelekeza jinsi ya kupiga kura....

Tukutane Jumapili Dar Live
1.Emmy Kosgei-Kenya
2.Dena Mwana – Congo
3.Ntokozo Mbambo- South Africa
4.Rebecca- UK
5.Gifty Osei- Ghana
6.Kefee -Nigeria
7.Onos Ariyo- Nigeria
8.Diana Hamilton-UK
9.Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria
VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA-MSIKILZE SHUSHO ALIPOKUWA ANAONGEA NA MABLOGAZ JANA THE ATRIUMS HOTEL SINZA AFRIKASANA
USIKOSE MTUMISHI WA MUNGU...NJOO TUFANYE KAZI YA BWANA KWA KUM-SUPPORT MTANZANIA MWENZETU 

KAMA ULIKUWA HUJUI KUHUSIANA NA MASHINDANO HAYA, TAFADHALI SOMA HAPO CHINI



Siku 18 zimebakia kabla ya pazia la upigaji kura kufungwa kwa waimbaji wa gospel barani Afrika, ambao wanawania tuzo mbalimbali kupitia Africa gospel music awards ambazo zinatarajiwa kutolewa siku ya jumamosi ya tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza. Ambapo kama ilivyokuwa kwa mwaka jana mwimbaji wetu mmoja tu, ametutoa kimasomaso kwa kupendekezwa katika kuwania kupata tuzo hizo mwimbaji huyo si mwingine bali ni Christina Shusho, ambaye mwaka jana alitoka mikono mitupu lakini mwaka huu tukiungana kwa pamoja watanzania wote kwa kumpigia kura lazima atarudi na tuzo zote mbili alizopendekezwa kuwania.

Shusho yumo kwenye kuwania mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na mwimbaji bora wa mwaka Afrika ya mashariki, tuzo ambazo anawania na waimbaji wengine wanaofanya vyema kwenye gospel barani Afrika wakiwemo wakina Ntokozo Mbambo wa Afrika ya kusini na waimbaji wengine. Kikubwa ninachoweza kukwambia tukifanikiwa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kwa kumpigia kura atakuwa nanafasi kubwa ya kutwaa tuzo hizo, kwasababu waimbaji wengine wanaowania tuzo hizo wengi wao wanatoka nchi moja hali ambayo itafanya kura zao kugawana kitu ambacho kitatupa nguvu ya kumwezesha Shusho kurudi na tuzo kwani Tanzania nzima kura zetu tunaelekeza kwake.

Mikakati mbalimbali inafanywa ili kuhakikisha kila mtu anashiriki katika upigaji kura kwakuwa hauhitaji kulipa ili kupiga kura, kikubwa unatakiwa ujiandikishe kwenye tovuti ya shindano hilo ambayo maelekezo yake yapo chini ya habari hii, zaidi kama nilivyoandika mikakati inafanywa ili kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili katika siku 18 zilizobaki. Hapo jana bloggers walikutana na Christina Shusho katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ili kupanga mikakati zaidi ya kuweza kupata tuzo hizo ambazo faida yake ni kumwinua Yesu pamoja na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania duniani. Natumai umenielewa ili kupiga kura ingia kwenye link hii na kufuata maelekezo chini yake.
http://www.africagospelawards.com/nominate.html


AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the 'VOTE NOW' button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.


ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA BLOGGERS NA CHRISTINA SHUSHO HAPO JANA 
Kikao kikiendelea

Blogger Victor kulia akinukuu jambo kutoka kwa Christina Shusho
Rulea Sanga alipoamua kupiga picha ya pamoja
Shusho akieleza jambo kwa mabloggers
 Victor akizidi kuchangia nawazo yake
K-Junior akiwa busy na kuchukua maphotoz

Watumishi wa Mungu wakihakikisha kila kitu kinaenda sawa


Papaa akimuelezea Shusho mikakati ya mabloggerz kuhusiana na upigaji kura


Kutoka kulia ni Shusho, Martin Malecela pamoja na Victor Mboya wakimsikiliza Rulea Sanga akimpongeza Shusho kwa juhudi zake


Rulea Sanga akisikiliza kwa makini mchakato wa kupata tuzo ulivyo.


Mablogaz  na mchungaji aliyoko upande wa kulia


K-junior wa kwanza upande wa kulia akimsikiliza mchungaji wa Vijana


Hakika kikao kilinoga wajameni.

Unclejimmy


Kikako kikiendelea na mabloggerz Tanzania waliojikita kumtangaza Kristo

''Inuka maana shughuli hii yakuhusu wewe, uwe na moyo mkuu, ukaitende (Ezra 10;4)''.
VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA.

Sunday, May 20, 2012


FADHAGET SANITARIUM CLINIC CD KUPATIKA SASA-Dr. Fadhili Emily
Dokta Fadhili amesema sasa unaweza kupata mafundisho kuhusiana na huduma za tiba zinazotolewa na Sanitarium Clinic iliyoko Mbezi Beach Tangi Bovu, Tandika Majaribio-Dar es Salaam Tanzania

Amewaomba watu wote kununua CD hii ili uweze kujifunza ni jinsi gani unaweza ukatibiwa magonjwa sugu kwa njia ya mimea na matunda.

Kama ungependa kujua zaidi jinsi ya kupata hizi CD, tafadhali wasiliana nasi kwa mawasiliano yaliyopo katika CD hapo chini:-




CD case imetengenezwa na Rulea Sanga +255 715 85 15 23 | rumatz2011@yahoo.com | www.rumaafrica.blogspot.com
UZINDUZI WA ALBUM YA "USILIE" YA THE VOICE OF HEALING CHOIR YA CHUO CHA MZUMBE-MOROGORO KUFANYIKA LEO 18 MEI 2012 CHUONI HAPO

Uzinduzi huo utaanza saa 8:00 usiku katika chuo cha Mzumbe kwa lengo la kuzindua albamu yao ya pili ya Usilie.

Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mh. Mtata ambaye ni mheshimiwa. mwenye umri mdogo sana, na inasemekana hata miaka 30 hajafikisha na siku mbili tatu zimepita tanguia ameteuliwa na raisi kuwa Mkuu wa Wilaya Kilombero. Na hii ndiyo kazi yake ya kwanza tangia aingie madarakani. "Chini ya Kapeti-Bado hajaoa" na kingine ni kwamba amesoma katika chuo hicho cha Mzumbe.

Wageni wengine watakaokuwepo ni Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi, Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe, Waandishi wa Habari , Afisa Tawala wa Wilaya, Mwambeni, Blogger wenu Rulea sanga na wengine wengi.

Kumbuka mshereheshaji wa shughuli hiyo ni Mchungaji Haris Kapiga na mtangazaji wa redio ya Clouds FM jijini Dar es Salaam

Vifaa vya muziki ni kutoka katika kikundi cha Glorious Celebratio kilichoko Dar es Salaam, chini ya Askofu Mwakanga'ta wa kanisa la The Victory Church.

Mpigaji picha na atakyerusha habari zote ni Blogger na Graphic Designer, Rulea Sanga ambaye ni meneja masoko wa Glorious Celebration

Kutakuwa na waimbaji mbalimbali kama Sarah ambaye ni mwanafunzi katika chuo cha biashara India, Glorious Celebration, Wanachuo cha Mzumbe na wengine wengi

GLORIOU CELEBRATION WAKIWA SAFARINI KUELEKEA MOROGORO KUWASINDIKIZA NDUGU ZAO KATIKA UZINDUZI.

Ngoja tuone safari nzima ya watumishi wa Mungu, Glorious Celebration
Blogger Rulea Sanga wa pili kutoka kulia nikijiongezea maarafa kwa kujisoma kitabu cha Nabii TB Joshua "The Mirror"
Blogger na Graphic Designer, Rulea Sanga nikiwa na GC maeneo ya Morogoro Stand
Mpoki wa Ze Commedy alitubamba Morogoro Stand
Blogger Rulea Sanga nikiwa kazini
Nice (kushoto) na Davina (kulia)
Glorious wakiangalia tangazo la tamasha Mzumbe
Angel Bernard (kushoto) na Mercy wakiwa ndani ya ukumbi
Emmanuel Mabisa (kushoto) na Sarah Shilla
Chaka akirekebisha mitambo (Technician wa Glorious Celebration)
Mwimbaji wa Glorious Celebration, Paul akijaribu MIC
Technician wa Glorious Celebration, Aron akihakikisha mitambo inaenda sawa

Wapigaji gitaa wa Glorious Celebration wakiihakikisha mambo yanaenda sawa

KABLA YA YOTE MISOSI ULIPEWA KIPAUMBELE SANA
 Graphic Designer na Blogger wenu, Rulea Sanga sikuwa mbali sana na kitu cha Mbeya
 Waimbaji wa Glorious Celebration (GC), Kulia na Immanuel Malisa
Waimbaji wa Glorious Celebration David (kushoto) na Paul
KAZI IKAANZA
---------------------------------------
THE VOICE OF HEALING CHOIR WAKIINGIA UKUMBINI
 The Voice of Healing Choir wakiingia ukumbini kwaajili ya uzindizi wa albamu yao ya Usilie Vol 2




Kwaya ya wanachuo-Mzumbe











 Mwimbaji wa nyimbo za injili anayesoma India, Sarah...hakukosa usiku huo

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero ambaye alikuwa mgeni rasmi, Mh. Mtata akiipita risala iliyosomwa na mmoja wa waimbaji wa The Voice of Healing Choir

waziri wa mambo ya ndani, Nchimbi akisalimia na mmoja wa wachungaji katika kipindi cha kuizindua albamu hiyo na kuiombea

 Mshereheshaji Haris Kapiga akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani, Dr Nchimbi kipaza
 Kulia ni mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe akimsikiliza mgeni rasmi

 Maombezi yakiendelea
 Wana kwaya ya The Voice of Healing wakiwa katika maombezi
 Wanachuo wakiwa katika maombi
Glorious Celebration wakioombea albamu ya Usilie


Baada ya maombezi wageni rasmi wakiwa wanaangalia uimbaji

Mkuu wa Chuo Cha Mzumbe


Kutoka kulia ni Davina, Nice, Mercy, Angel
Paul aki-lead
Mtalamu wa Drumkatika kikundi cha GC
Imma solo akisaka Solo